Kifungu cha 20(1) cha Sheria Namba18 ya Mwaka 2009 ya Korosho na Kanuni za Mwaka 2010 kinabainisha kwamba Bodi ya Korosho Tanzania ndiye msimamizi Tasnia ya Korosho nchini. Pamoja na mambo mengine, Bodi ya Korosho inasimamia udhibiti wa ubora wa Korosho ghafi, karanga na bidhaa zote zitokanazo na Korosho.
Kwa mwaka huu, Bodi ya Korosho inaendesha mafunzo ya uhakiki ubora kwa watu wote wanaofanya kazi ama wenye nia ya kufanya kazi za uhakiki ubora katika msimu wa mauzo ya Korosho kwa mwaka 2020/2021. Mafunzo hayo yanalenga wataalam wapya na wale wanaoongeza ujuzi (kwa waliowahi kupatiwa mafunzo kabla). Mafunzo haya ni muhimu kwa wadau mbalimbali wakiwamo Waendesha Ghala, Wanunuzi, Vyama Vikuu vya Ushirika na Wamiliki wa Viwanda vya kubangua Korosho, wataalam wa ugani na kilimo.
Mafunzo yameanza kufanyika tarehe 01/09/2020 hadi 05/09/2020 katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Kilimo Mtwara (MAT).
Sifa za Mshiriki:
Bodi ya Korosho kwa niaba ya Chama Kikuu cha ushirika RUNALI inapenda kukutaarifu mabadiliko ya eneo la mnada wa tarehe 25.10.2020 ambao ilikua ufanyike wilaya ya Liwale kwa siku ya tarehe 25.10.2020 badala yake mnada huo utafanyika wilaya ya Nachingwea kwenye ofisi za RUNALI.
Kwa niaba ya Bodi ya chama kikuu RUNALI Bodi ya Korosho inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza aidha inapenda kukualika kuhudhuria mnada huo utakaoanza saa 3:00 asubuhi hadi 10:00 jioni bila ya kukosa.
Director General
Cashewnut Board Of Tanzania
P.O BOX 533
Mtwara
Telephone (023) 2333303
Fax (023) 2333536
Email: info@cashew.go.tz
P.O BOX 9234
Dar Es Salaam
Telephone (022) 2113161
Fax (022) 2117918
Email: info@cashew.go.tz
P.O BOX 127
Tunduru
Telephone/Fax (025) 2680221
Email: info@cashew.go.tz
P.O BOX 1032
Lindi
Telephone 023-2202006
Email: info@cashew.go.tz
P.O BOX 119
Manyoni
Telephone 073881077
Email: info@cashew.go.tz