MKUTANO WA 13 WA KOROSHO WA ACA KUFANYIKA INCHINI TANZANIA

Tanzania inategemewa kuwa mwenyeji kwenye mkutano wa 13 wa korosho wa ACA ambao unatarajiwa kufanyika mapema mwezi November mwaka huu katika ukumbi wa Mikutano wa Julias Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema, mwakilishi wa Wizara ya Kilimo, Dk. Steven Ngailo, amesema mkutano huo umelenga kuzungumzia mada muhimu ikiwemo utungaji sera na changamoto katika sekta ya korosho katika utekelezaji wake ubunifu wa ubanguaji korosho, utafiti wa uzalishaji pamoja na uwekezaji katika tasnia ya Korosho Afrika.

Kwa upande wake, Mkurungezi mkuu wa Africa cashew Alliance Mr Ernest Mintah amesema kuwa, mkutano huo wa mwaka utafanyika kwa ushirikiano wa wa ofisi za serikali ya Tanzania kwa kuzingatia sheria zinazodimamia sera zinazohusiana na korosho nchini Tanzania

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Francis Alfred amesema kuwa, mwaka huu malengo ni kuchambua mabadiliko ya sasa ya soko, mwitikio wa serikali na watendaji wa mnyororo wa thamani na kuchanganua wajibu wa wadau wote wa umma na binafsi katika kushughulikia masuala yanayojitokeza