Kaimu mkurugenzi mkuu ajadiliana na Wenye viwanda vya kubangua Korosho

Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania amejadiliana na wenye viwanda vya kubangua korosho nchini. Kikao hicho kilichofanyika Dar es Salaam katika ukumbi wa TIC tarehe 24 Agosti, 2019 kilikua na Lengo la kujadili namna ya kuongeza mchango wa wabanguaji katika ustawi wa tasnia ya korosho nchini.