UZINDUZI WA MAFUNZO YA MATUMIZI BORA YA VIUATILIFU

Mafunzo ya matumizi bora ya viuatilifu

Bodi ya Korosho Tanzania imezindua mafunzo ya matumizi bora na sahihi ya viuatilifu vya Korosho.

Madhumuni ya mafunzo haya ni kuongeza tija na ubora wa zao la korosho ili kukuza pato la mkulima na Taifa kwa ujumla. Utekelezaji wa madhumuni haya utazingatia malengo yafuatayo:-

  1. i. Kuwafundisha wakulima wa korosho, wapuliziaji wa mikorosho na maafisa ugani waliopo katika maeneo yanayolima korosho mbinu za kilimo bora cha korosho hususani utambuzi na matumizi sahihi ya viuatilifu.
  2. ii. Kuhamasisha matumizi ya viuatilifu vya zao la korosho dhidi ya magonjwa na wadudu waharibifu ili kuongeza tija katika uzalishaji wa korosho nchini.
  3. iii. Kuwakumbusha wakulima kuendelea kujipatia huduma ya viuatilifu vilivyosajiliwa na TPRI na vinavyosambazwa na Bodi ya Korosho na Vyama Vikuu vya Ushirika kutoka vituo mbalimbali vilivyopo nchini.
  4. iv. Kuwajengea uwezo maafisa ugani/kilimo wapya walioajiriwa katika Halmashauri zinazozalisha korosho ili waweze kutimiza wajibu wao ipasavyo.