MAFUNZO YA UBORA WA KOROSHO MSIMU 2019/2020

 • Bodi kuendesha mafunzo ya uhakiki ubora msimu wa mwaka 2019. Download in PDF
 • Kifungu cha 20(1) cha Sheria Namba18 ya Mwaka 2009 ya Korosho na Kanuni za Mwaka 2010

  Bodi ya Korosho Tanzania ndiye msimamizi Tasnia ya Korosho nchini. Pamoja na mambo mengine, Bodi ya Korosho inasimamia udhibiti wa ubora wa Korosho ghafi, karanga na bidhaa zote zitokanazo na Korosho.

  Kwa mwaka huu, Bodi ya Korosho itaendesha mafunzo ya uhakiki ubora kwa watu wote wanaofanya kazi ama wenye nia ya kufanya kazi za uhakiki ubora katika msimu wa mauzo ya Korosho kwa mwaka 2019/2020. Mafunzo hayo yanalenga wataalam wapya na wale wanaoongeza ujuzi (kwa waliowahi kupatiwa mafunzo kabla). Mafunzo haya ni muhimu kwa wadau mbalimbali wakiwamo Waendesha Ghala, Wanunuzi, Vyama Vikuu vya Ushirika na Wamiliki wa Viwanda vya kubangua Korosho, wataalam wa ugani na kilimo.

  Mafunzo yatafanyika kuanzia tarehe 11/10/2019 hadi 15/10/2019 katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Kilimo Mtwara (MAT).

  Sifa za Mshiriki:

  • Msimamizi wa kitengo cha ubora: Awe na astashahada ya kilimo au fani yoyote inayoshabihiana na hiyo kutoka chuo chochote kinachotambulika kitaaluma.
  • Supporting stuff: Awe na elimu ya kuanzia kidato cha nne na uzoefu.

  Gharama ya mafunzo na cheti ni sh. 200,000/= malipo yote yafanyike kupitia benki:

  Benki: CRDB, Tawi la Mtwara, Jina la Akaunti: Cashewnut Board of Tanzania.

  Akaunti namba 01J1015826005. Mwisho wa kupokea malipo ni tarehe 09/10/2019 saa 10:30 jioni, baada ya kulipia hakikisha unatuma nakala ya hati ya malipo ya benki kwa barua pepe info@cashew.go.tz .

  Bodi inasisitiza kuwa hakuna mtaalam yoyote wa ubora atakayeruhusiwa kufanya kazi za uhakiki ubora wa korosho ghafi kwa msimu 2019/2020 kwenye ghala za minada, ghala za Wanunuzi na Viwanda vya kubangua korosho ghafi kama hajapatiwa mafunzo na cheti kutoka Bodi ya korosho.

  Aidha, Wataalam kwenye ghala wenye vyeti vya mwaka 2018/2019 pamoja na mameneja wa ghala zote Tanzania watawajibika kuhudhuria bila kukosa siku ya tarehe 15/10/2019 kwaajili ya kupata update za msimu 2019/2020 kwa gharama ya 50,000/= kwa kila mmoja kwa account tajwa hapo juu. Kwa maelezo zaidi fika katika ofisi za Bodi ya Korosho Tanzania HQ –Mtwara, Lindi, Tunduru, Dar es salaam, Tanga, Mnyoni na Morogoro

  Download in PDF