Bodi yatoa pikipiki nne kwa Halmashauri ya wilaya ya Manyoni

Bodi ya Korosho Tanzania imetoa pikipiki nne kwa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni. Pikipiki hizo zitatumika na maafisa ugani kwa ajili ya kurahisisha na kuongeza tija na ufanisi katika shughuli zao za kila siku.
Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Francis Alfred alikabidhi pikipiki hizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri mbele ya Mbunge wa jimbo la Manyoni Kaskazini , Meneja wa Bodi ya Korosho tawi la Manyoni pamoja na Maafisa wengine wa serikali.
Akiwa wilayani humo pia Bwn. Alfred pia alitembelea shamba la pamoja la Korosho maarufu kama block farm lenye ukubwa wa ekari takriban 12,000 ambapo hadi sasa ekari zipatazo 7000 zimepandwa mikorosho na ekari 5000 zikiwa kwenye maandalizi ya awali.