Bodi yatoa Muongozo wa utaratibu wa ukopeshaji wa viuatilifu

Pakua Muongozo wa utaratibu wa ukopeshaji wa viuatilifu

Bodi imetoa Mwongozo wa utaratibu wa ukopeshaji wa viuatilifu vya zao la korosho vinavyouzwa na bodi ya korosho tanzania msimu wa 2019/2020

Mwongozo huu unaainisha vipengele vifuatavyo :-

 • i.
 • 1. Mkopo huu ni wa hiari na ni kwa Mkulima wa Korosho anayeuza korosho zake kupitia Chama cha Ushirika cha Msingi cha Mazao (AMCOS).

  2. Viuatilifu vinavyokopeshwa ni vile vinavyouzwa na Bodi ya Korosho Tanzania msimu wa 2019/2020 (Kiambatisho Na. 1).

  3. Mkopo huu ni wa nusu bei (50%), ambapo nusu italipwa na Mkulima mwenyewe wakati wa kuchukua viuatilifu na nusu inayobaki itakatwa kutoka kwenye mauzo ya korosho za mkulima husika msimu wa 2019/2020.

  4. Mkulima atatakiwa kulipia na kupewa kiasi cha viuatilifu vilivyoidhinishwa na kupitishwa na Bodi ya Korosho Tanzania.

  5. Mkulima anayehitaji Mkopo wa viuatilifu anatakiwa awe amesajiliwa na Bodi ya Korosho Tanzania kwenye daftari la kudumu la wakulima wa korosho.

  6. Mkulima ambaye hajapata malipo ya korosho za msimu wa 2018/2019 anaweza kuomba mkopo wa 100% kwa sharti la 50% kukatwa kutoka kwenye fedha za malipo ya
  korosho za msimu wa 2018/2019. Asilimia 50 inayobaki itakatwa kutoka kwenye mauzo ya korosho za msimu wa 2019/2020.
 • ii.
 • 1. Mkulima anayehitaji mkopo wa viuatilifu anatakiwa kwenda katika Chama cha Msingi (AMCOS) anachouzia korosho wakati wa msimu ambapo atachukua na kujaza fomu ya maombi ya mkopo. Fomu hiyo ni lazima ipitishwe na Mtendaji wa Kijiji/Kata atakayekuwa na jukumu la kumtambua mkulima huyo na kuhakikisha kuwa anauza korosho zake za msimu wa 2019/2020 kupitia AMCOS aliyochukulia mkopo.

  2. Chama cha Msingi kitapitia na kuchambua maombi ya mkopo kwa kujiridhisha kuwa mwombaji ni mkulima wa korosho na wakati wa msimu wa 2019/2020 korosho zake atauzia kupitia chama hicho.

  3. Mara baada ya uchambuzi, Chama cha Msingi kinatakiwa kuandaa orodha ya wakulima wanaokidhi vigezo ikiainisha jina kamili la mkulima, kijiji, kata, Halmashauri, Akaunti namba na Benki, Namba ya Simu ya Mkononi, Kiasi na Aina ya viuatilifu anavyohitaji kukopa ikiwa ni pamoja na thamani yake, na Ghala la kuchukulia Viuatilifu hivyo. Kiambatisho Na. 1 kinaonesha aina na bei ya viuatilifu vinavyosambazwa na Bodi ya Korosho Tanzania msimu wa 2019/2020. Kiambatisho Na. 2 kinaonesha maghala/vituo vya usambazaji wa viuatilifu vya Bodi ya Korosho Tanzania msimu wa 2019/2020.

  4. Chama cha Msingi kitaandaa barua ya maombi ya mkopo wa viuatilifu kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania kupitia Meneja Mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika (Union) husika ikiambatishwa na orodha ya wakulima husika na muhtasari wa kikao cha Bodi ya Chama cha Msingi kuridhia wakulima hao kukopeshwa viuatilifu hivyo.

  5. Chama Kikuu kitapitia na kuchambua maombi husika kabla ya kuwasilisha mapendekezo ya wakulima wanaostahili kukopeshwa viuatilifu kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania.

  6. Bodi ya Korosho Tanzania itapitia maombi husika ikiwa ni pamoja na kuona kuwa wakulima waliopo kwenye orodha ya maombi ya mkopo wa viuatilifu ni miongoni mwa wakulima waliosajiliwa.

  7. Bodi ya Korosho Tanzania itapitisha mkopo wa viuatilifu kwa wakulima husika kulingana na kiasi cha viuatilifu vitakavyokuwepo maghalani wakati huo.

  8. Bodi ya Korosho Tanzania itatoa taarifa ya wakulima walioidhinishwa kupata mkopo wa viuatilifu kwa kila Chama cha Msingi kupitia Chama Kikuu husika.

  9. Chama cha Msingi kitawapa taarifa wakulima ambao maombi yao yameidhinishwa na kuwataka kwenda kulipia malipo ya awali (50%) kwenye Benki ya NMB au mawakala wake kupitia Akaunti Na. 71310008327 ya Bodi ya Korosho Tanzania. 10. Mara baada ya malipo mkulima husika atatakiwa kwenda na risiti ya malipo ya benki (Pay-in-slip) pamoja na kitambulisho (Mpiga kura/Taifa/Leseni ya udereva) kwenye kituo cha usambazaji wa viuatilifu vya Bodi ya Korosho Tanzania kilichopo karibu yake kwa ajili ya kupewa stakabadhi na kuchukua viuatilifu husika.

  11. Bodi ya Korosho Tanzania itatakiwa kuandaa orodha ya wakulima waliochukua mkopo na thamani yake kwenda kwa Meneja Mkuu wa Chama Kikuu husika kwa ajili ya makato ya 50% ya mkopo kutoka kwenye malipo ya mauzo ya korosho msimu wa 2019/2020.

  12. Chama Kikuu kitatakiwa kuhakikisha kuwa fedha hizo zinakatwa wakati zikiwa kwenye akaunti ya pamoja (Collection Account) ya mauzo ya korosho na kisha kuziweka katika akaunti ya pembejeo ya Bodi ya Korosho Tanzania iliyopo Benki ya NMB.

  13. Bodi ya Korosho Tanzania itatoa stakabadhi kukiri fedha husika zimewekwa katika Akaunti ya Pembejeo na hivyo kufuta deni la mkulima/wakulima husika.
 • iii.
 • Utekelezaji wa Mwongozo huu ni kwa msimu wa 2019/2020.
 • iv.
 • Serikali haitawajibika kwa namna yoyote ile kwa mdau/mhusika ambaye hatazingatia utaratibu uliowekwa kwenye Mwongozo huu.