Wanunuzi wa Korosho kupata leseni na vibali Online msimu huu

Utaratibu wa kuomba na kupata leseni na vibali Online    ATMIS

Utaratibu wa kujisajili, kuomba leseni na vibali kupitia mfumo wa wizara ya kilimo wa kusimamia biashara za kilimo (ATMIS) kwa wanunuzi wa zao la korosho msimu wa mwaka 2019/20

 • i.
 • Andika anuani ya mfumo https://atmis.kilimo.go.tz. Kwenye program yako ya kuingilia kwenye mtandao wa tovuti (Kielelezo Na. 1)

  ... Kielelezo Na. 1: Namna ya kuingia kwenye mfumo wa ATMIS
 • ii.
 • Kwenye Orodha ya Taasisi mbalimbali chagua na ubonyeze Cashewnut Board Of Tanzania (Kielelezo Na. 2)

  ... Kielelezo Na. 2 : Jinsi ya kuchagua Bodi ya Korosho kwenye Orodha ya Taasisi mbalimbali zilizomo kwenye mfumo wa ATMIS

   Bonyeza Register Online ili ufungue fomu ya kujiandikisha taarifa zako kwenye mfumo wa ATMIS (Kielelezo Na. 3)

  ... Kielelezo Na. 3: Namna ya kuingia ili kujisajili online

   Jaza taarifa zinzohitajika pamoja na viambatisho vinavyotakiwa ambavyo ni

  • i. TIN
  • ii. Certificate of Incorporation
  • iii. Bussiness license
  • iv. VAT Registration Certificate
  Kumbuka kuhifadhi username na password yako ya kuingilia kwenye mfumo (Kielelezo Na. 4)

  ... Kielelezo Na.4 : Fomu ya usajili wa mnunuzi

 • iii.
  • Login kwenye mfumo kwa kuandika username na password
  • Ukiingia kwenye mfumo chagua Applications
  • Jina la Taasisi (Organization) - chagua Cashewnut Board Of Tanzania na kisha chagua aina ya leseni/kibali unachotaka (Kielelezo Na 5)
  ... Kielelezo Na. 5 : Namna ya kuingia kwenye sehemu ya kupata leseni/ vibali
 • iv.
 • Taratibu za kiofisi zikikamilika, kibali kitapatikana kwenye mfumo huu wa ATMIS ambapo kinaweza kupakuliwa (downloaded) na Mnunuzi anaweza akakichapisha mwenyewe kwenye printa yake akiwa mahali popote.

  • Upande wa kushoto kwenye Menu bonyeza Permits/License/ Certificates (Kielelezo Na 6)
  ... Kielelezo Na. 6 : Namna ya kuingia kwenye sehemu ya kupata leseni/ vibali

  • Kwenye Organization chagua Cashewnut Board of Tanzania (Kielelezo Na 7)
  ... Kielelezo Na 7: Namna ya kuchagua taasisi ili kupata vibali

  • Baada ya kuchagua Organization chagua aina ya kibali/ leseni uliyoomba ili uipakue na kuiprint au kama bado haijatoka uone hatua ilipofikia (status) (Kielelezo Na 8)
  ... Kielelezo Na. 8 : Namna ya kupata kibali ulichoomba

   Kibali kitakua kwenye mfumo wa nakala laini ambayo mnunuzi anaweza akaprint

 • v.
  • Leseni ya ununuzi wa Korosho kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi
  • Leseni ya ununui wa Korosho kwa ajili ya kubangua ndani ya nchi
  • Kibali cha kusafirisha Korosho zilizobanguliwa ndani ya nchi
  • Kibali cha kusafirisha Korosho nje ya nchi (Export permit)
 • v.
 • Makampuni ya nje ambayo hayajasajiliwa hapa nchini yanaweza kushiriki katika minada kwa kuingiamakubaliano maalum na Benki, zinazotambuliwa na Soko la Bidhaa hapa nchini (TMX) Tovuti: www.tmx.co.tz Barua Pepe: info@tmx.co.tz
 • Download these instructions in PDF

 • Pakua maelezo kwenye PDF katika lugha ya Kiswahili