ZOEZI LA USAJILI WA WAKULIMA

Afisa wa Bodi ya Korosho akizungumza na wakulima wa Korosho katika zoezi la ukusanyaji wa Fomu za usajili wa wakulima

Bodi ya Korosho Tanzania inapenda kuwatangazia wakulima wa Korosho kuwa zoezi la usajili wa wakulima bado halijafungwa. Wakulima ambao bado hawajajaza fomu za taarifa zilizoandaliwa na kusambazwa na Bodi ya Korosho wanatakiwa kujaza fomu hizo na kuzirejesha kwa mtendaji wa kijiji au kata.

Wakulima wanasajiliwa ili kurahisisha mipango ya mendeleo kwa wakulima wa zao la Korosho.