14 Aug, 2026
admin
Habari na Matukio
UJUMBE WA OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI WATEMBELEA CBT, MRADI WA KONGANI YA VIWANDA MARANJE
Ujumbe kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, agosti 14, 2026 umetembelea Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), ambapo walipata fursa ya kufahamu shughuli mbalimbali za Bodi pamoja na kushuhudia maendeleo ya Mradi wa Kongani ya Viwanda Maranje unaotekelezwa katika kijiji cha Maranje, Halmashauri ya Mji Nanyamba, Mkoa wa Mtwara.
Wakiwa katika kongani ya viwanda walipata Fursa ya kujionea na kujifunza namna uwekezaji katika kongani ya viwanda unavyofanyika na uzingativu wa masuala ya kisheria katika Uwekezaji.
Ujumbe huo uliambatana na baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya Bodi ya Korosho Tanzania ambao walitoa maelezo kuhusu hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi na umuhimu wake katika kuongeza thamani ya zao la korosho.
Lebo: