WADAU WA TASNIA YA KOROSHO WAKUTANA MKOANI MOROGORO
Wadau mbalimbali wa Tasnia ya Korosho, wakiwemo wakulima, wafanyabiashara, wabanguaji wa korosho, wawakilishi wa Serikali, taasisi za utafiti, vyama Vikuu vya Ushirika pamoja na wadau wengine katika mnyororo wa thamani wa korosho, wamekutana mkoani Morogoro Agosti 27, 2026, kujadili changamoto, fursa na mikakati ya kuendeleza na kuimarisha Tasnia ya Korosho nchini.
Mkutano huo uliongozwa na Mheshimiwa Adam Malima, aliyemwakilisha Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Daniel Chongolo.