Skip to main content
BODI YA WAKURUGENZI YA BODI YA KOROSHO YAFANYA KIKAO CHA SABA
11 Oct, 2026
admin
Habari na Matukio

BODI YA WAKURUGENZI YA BODI YA KOROSHO YAFANYA KIKAO CHA SABA

MTWARA

Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) imefanya Kikao cha Saba (07) tarehe 10 Oktoba, 2026, katika Ukumbi wa Mikutano wa Bodi hiyo, Mtwara. Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Brig. Gen. (Mstaafu) Aloyce D. Mwanjile, NDC, kikihudhuriwa na wajumbe wa Bodi pamoja na Menejimenti ya Bodi wakiwa waalikwa.

Katika kikao hicho, Bodi imepitia na kujadili Muhtasari wa Kikao cha Sita (06) cha Bodi ya Wakurugenzi kilichofanyika tarehe 20 Julai, 2026, pamoja na taarifa ya utekelezaji wa maazimio na maelekezo yaliyotolewa katika kikao hicho, kwa lengo la kufuatilia hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa maamuzi ya Bodi.

Aidha, kikao kimepitia taarifa zilizowasilishwa na Kamati mbalimbali za Bodi, ambazo ni Kamati ya Utendaji, Kamati ya Uendelezaji Zao la Korosho, pamoja na Kamati ya Ukaguzi na Usimamizi wa Vihatarishi. Taarifa hizo zimewasilishwa na wenyeviti wa kamati husika kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi kwa ajili ya kupitiwa, kujadiliwa na kutolewa maelekezo stahiki.

Kikao hicho ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya Bodi ya Wakurugenzi katika kusimamia na kuelekeza shughuli za Bodi ya Korosho Tanzania, kwa kuzingatia utawala bora, uwajibikaji na usimamizi madhubuti wa tasnia ya korosho nchini.

Lebo: