MAREKEBISHO YA SHERIA YA TASNIA YA KOROSHO KUIMARISHA USIMAMIZI NA UHALISIA WA SASA WA TASNIA YA KOROSHO NCHINI
MOROGORO
Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) imefanya kikao cha kujadili na kupitia marekebisho ya Sheria ya Tasnia ya Korosho, hatua inayolenga kuboresha na kurekebisha sheria ya Tasnia ya Korosho ili kuendana na Uhalisia wa sasa pamoja na kuimarisha mfumo wa kisheria katika usimamizi wa Tasnia ya Korosho nchini.
Kikao hicho kimewakutanisha wajumbe wa Menejimenti ya Bodi ya Korosho Tanzania pamoja na Mawakili wa Serikali kutoka Taasisi na Halmashauri mbalimbali huku majadiliano yakilenga kupitia kwa kina maeneo mbalimbali ya sheria yanayohitaji kufanyiwa marekebisho ili yaendane na mahitaji na mabadiliko ya sasa katika uzalishaji, uongezaji thamani, biashara na maendeleo ya tasnia ya korosho.
Aidha lengo kuu ni kufanya maboresho katika vifungu na masharti ya sheria iliyopo ili kuifanya iendane na mazingira, mahitaji na changamoto za sasa za tasnia, hatua inayotarajiwa kuimarisha usimamizi na uratibu wa shughuli mbalimbali kuanzia Uzalishaji, Ubora, Ubanguaji, Uhifadhi na Masoko.
Kikao hicho kimefanyika agosti 24, 2026 katika ukumbi wa hoteli ya Morena mkoani Morogoro kikiongozwa na Ndg. Gilbert Rweyemam, Afisa Sheria kutoka Bodi ya Korosho Tanzania.