Skip to main content
MKURUGENZI MKUU CBT AWAFARIJI FAMILIA YA MKULIMA WA KOROSHO ALIYEFARIKI KWA AJALI YA MOTO MASASI
16 Aug, 2026
admin
Habari na Matukio

MKURUGENZI MKUU CBT AWAFARIJI FAMILIA YA MKULIMA WA KOROSHO ALIYEFARIKI KWA AJALI YA MOTO MASASI

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Francis Alfred, agosti 15, 2026 ametembelea na kutoa pole kwa familia ya marehemu Fatuma Mkopoka mkulima wa korosho aliyefariki dunia baada ya kupatwa na ajali ya moto wakati akisafisha shamba lake la korosho katika Kata ya Ndanda, Wilaya ya Masasi, Mkoa wa Mtwara.

Katika ziara hiyo, Mkurugenzi Mkuu alifika katika Kijiji cha Njenga, ambako marehemu alikuwa akiishi, kwa ajili ya kuwafariji ndugu, jamaa na familia ya marehemu kufuatia msiba huo. 

Mkurugenzi Mkuu aliambatana na Afisa Kilimo wa CBT kutoka Mtwara, Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Mwenyekiti wa Kijiji cha Njenga, Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Njenga, Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Masasi anayehudumia kata ya Ndanda pamoja na Afisa Kilimo wa mpango wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT).

Unaweza pia kutufuatilia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, Instagram na Threads ni @Cashewnutboard, Facebook, LinkedIn na X ni Cashewnut Board of Tanzania, Youtube ni Cashewnut Boardtz na Tovuti ni www.cashew.go.tz au email info@cashew.go.tz na simu ni 0800 112 159 bure.

Lebo: